Mwili unapojizoesha kutumia oksijeni kidogo taratibu huitwa aklaimetazesheni
Watu hutofautiana kwa namna wanavyoweza kuzoea matumizi ya oksijeni kidogo miilini mwao kwa kasi tofauti.Kwa hiyo hakuna kanuni ileile inayokidhi haja ya kila mwenye mahitaji hayo bali miongozo.
Zaidi ya m.3000 kutoka usawa wa bahari,panda taratibu na ulale baada ya m.300 kila siku.Kupanda juu mchana kutwa si vibaya bora tu ushuke ukalale chini.(panda juu,lala chini).Endapo utaenda juu na huwezi kushuka,pumzika kwa siku moja ili uruhusu mwili wako kujipanga.
Huu huonekana ni upandaji wa taratibu sana.Baadhi ya watu huweza kupanda juu haraka mno pasi na mushkeli ingawa kwenye kundi lazima atatokea asiyeweza kutumia oksijeni kidogo kirahisi.Ni busara kuwa na utaratibu wa kulinda afya zao.Ratiba ya mapumziko ya siku 2 hadi 3 pia ni msaada mwingine.
Kuruka kwa ndege au kuendesha gari kwenda nyanda za juu humaanisha wengi wataathirika na magonjwa hatari ya milimani.
Ni busara kuwa na taarifa za njia za usafiri tupangazo kuzitumia kabla ya safari.
Itapendeza kuchora ramani inayoonesha mwinuko wa mahali utakapolala ukiwa safarini usiku.Kama hujui,uliza..Cha kusikitisha sana ni kwamba hakuna mbinu bora zaidi ya kubashiri ni lini utaugua magonjwa haya,hivyo ni busara kuchukua tahadhari.