Ni dhahiri shairi kwamba unaposoma sehemu hii una mpango kabla ya tukio au kuna kitu hakikuenda sawa.Vyovyote vile iwavyo, muhimu ni kutopata hofu kuu.Yafuatayo yatakusaidia katika dharura.
-Hakikisha kila mmoja yu salama-wewe mwenyewe, majeruhi yeyote na wengine kwenye kundi.Mmoja akiugua ugonjwa wa joto la chini la mwili maarufu kama hypothermia, kuna uwezekano mkubwa kwamba wengine pia wana huo ugonjwa.Nenda sehemu salama kama utalazimika.Usiwe muathirika mwingine.
-Pawe na mwangalizi mmoja.
-Kusanya taarifa unazozihitaji. Tumia MAHFIZ kama muongozo.
Mahali hasa la tukio.
Aina ya ajali.
Hatari zinazoweza kuwakabili waokoaji.
Fursa ya kufikia eneo la tukio.
Idadi ya majeruhi.
Zana hitajika.
-Toa taarifa.Utakavyohitaji msaada wa haraka, ndivyo itakavyokuwa salama yako.Radio na simu huweza kutofanaya kazi milimani.Eleza uko wapi hasa (ili wajue tatizo liliko).Eleza kwa makini.
-Wahudumie waathirika kwa huduma bora iwezekanvyo. Kipaumbele cha huduma kikitwe katika kiwango cha jeraha.Sanduku la huduma ya kwanza ya kawaida inatosha.Maneno ganguzi na ya mliwazo huweza kwenda pamoja.
-Andaa mpango wa uokozi-vyombo vya usafiri asilia, kichukuzi au helikopta.
-Hakikisha kila mmoja anapashwa joto hadi msaada upatikane – huweza kuwa dakika kadhaa, saa kadhaa au hata siku kadhaa.
Eneo la kutua kwa helikopta
• Tafuta eneo la ardhi imara (au hata mteremko wa chini ya nyuzi 10) ikiwa na kipenyo cha hatua 100.
• Ondoa vitu vinavyoweza kuhatarisha usalama wa helikopta wakati wa kutua (watu na vitu).
• Weka alama ya ‘H’ kwa kutumia mawe au utumie tochi au nguo yenye rangi inayong’aa kutoa taarifa ya eneo.
• Mtu mmoja asimame nje ya uwanja, nyuma ya upepo akionesha alama ya sura ya ‘Y’ kwa mikono.
• Usiende kwenye helikopta hadi uruhusiwe na wafanyakazi wa kwenye helikopta.