Kiasi kikubwa cha miale ya altravayoleti kwenye uwanda wa juu huweza kuunguza macho(kukiwishwa na mng’ao wa theluji) kama kichanga-jicho uwapatao watia weko(mafundi wa kuchomelea vyuma).
Pumzika,weka vitu vyororo/laini vya kinga ya macho,vilainishi na dawa za maumivu husaidia.miwani mizuri ya jua huhitajika kwenye barafu kwani hata kama kuna hali ya mawingu mile ya altraviyoleti hupenya.Chagua miwani iliyotengenezwa kwa ajili ya milima si ya starehe.Maelekezo ya aina yanaweza kutolewa na madaktari husika,
Lenzi inayoambatanishwa na mboni huweza kutumika lakini usafi hasa ni wa lazima ambayo ni ngumu kwenye nyanda za juu.Lenzi zitumikavyo kwa siku kisha kutupwa hufaa ila lazima ziondolewe usiku. Aina ya Upasuaji wa macho (laser refractive surgery) huudhoofisha uoni wako katika nyanda za juu ila hujirekebisha ushukapo.Usifanyiwe upasuaji huu muda mfupi kisha uende safarini, jipange na iwe kwa muda muafaka.
Matone ya damu nyuma ya jicho huweza kutokea (retinal haemorrhages), inayoweza kuathiri uoni.Si hatari mara nyingi na hutoweka baada ya wiki chache. Shuka chini ukipofuka kwenye jicho lolote ukiwa uwanda wa juu.
Kwenye uwanda wa juu:
• Vaa miwani ikiwa inang’aa.
• Ukipoteza miwani tumia maarifa upate ubao wa vitundu vidogo vya kutazamia.
• Hakikisha watumishi wana miwani za barafu na wanazivaa.
• Hakikisha unakuwa msafi ukimbatananisha lenzi kwenye mboni.
Maandalizi:
• Uwe na miwani ya barafu.
• Uwe na lenzi inayoambatanishwa kwenye mboni na majimaji ya kusafishia.
• Kama unahitaji maji uwe na ziada ya kubadilisha.
Kijana wa miaka 29 alitumia lenzi ambatanishi kwenye mboni zinazotupwa kila siku kwenye mlima Everest.Hakuzibadilisha kwa siku nne, siku akiwa kileleni alitumia miwani ya jua si gogo,Akiwa kwenye m.8600,alianza kupoteza uoni.Kwenye kilele hakuweza kuona manadhari wala kutembea akiona. Alisaidiwa kushuka chini.Alikiwishwa na theluji na maambukizi ya bakteria.Daktari akaondoa lenzi iliyoambatanishwa kwenye mboni ingawa uchunguzi huo uliyaacha macho yake yakiwa hayawezi kuona vizuri.Angweza hata kufa.