Waendao nyanda za juu hawana budi kujihami dhidi ya magonjwa ya miinuko mirefu.Zikitumika njia bora za kupambana nazo,si changamoto tena kwenye nyanda za juu,kinyume chake ni maafa.Hutia doa kwa mgonjwa na hata wenzake kwenye kikundi huporwa raha hali kadhalika.
Ukitafakari afya yako kila siku upandapo mlima,huo ni msaada binafsi mkubwa mno.Endapo utajua wazi yanayoendelea mwilini mwako ,utayaokoa maisha yako.Mengi hutokea mwilini mwako ukweapo mlima.
Watu wengi walioshuhudia taathira za nyanda za juu huweza kukueleza kuhusu maumivu ya kichwa,kushindwa kupumua,kulala hovyo na hata kutohisi njaa.Hizi ni dalili za magonjwa ya nyanda za juu AMS.Magonjwa haya ni mshtuko wa mwili si tishio la maisha.Endapo dalili zake zikikithiri na uendelee na safari bila tiba,majimaji ya ubongoni(HACE)au yale ya mapafuni(HAPE) huweza kutokea.Mgonjwa huweza kupoteza uhai ghafla.
Ambacho watu hawakijui ni kwamba utahitaji kukojoa zaidi, kushindwa kujimudu,kubadilika kwa uoni nahata makucha pia.
Ni matarajio yetu kuwa sura inayofuata, itakuelimisha zaidi kuhusu masaibu yako katika nyanda za juu na namna ya kukabiliana nazo.Baadhi ni kwa ajili ya mliwazo wako ilhali mengine huweza kukusababishia madhara makubwa nay a muda mrefu n ahata kupoteza uhai wako.Kujua yanayoendelea mwilini mwako ukwepo juu ni burudani na huweza kuwa motisha safarini.Laiti ungejua jinsi mwili ulivyo makini kujihami na kujisawiri kwenye mabadiliko makubwa ya kimazingira upandapo,hakika ungehamasika kudadisi zaidi.